Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema ana furaha kuona mashabiki wa Arsenal hatimaye walipata jambo la kusherehekea baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Manchester United.

Ushindi huo wa Arsenal ulikuwa wa kwanza wa Arsene Wenger katika mechi 16 za ushindani dhidi ya timu iliyokuwa chini ya Mourinho.

Mourinho amesema kuwa “Niliondoka Highbury na walikuwa wanalia, nikaondoka Emirates na walikuwa wanalia lakini mechi hii wanashangilia ninafurahi pia.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Hatimaye leo (jana) mashabiki wa Arsenal wanaweza kuimba, wanarusha skafu hewani. Ni jambo zuri kwao.”

Pia ameongeza kwa kusema “Ni mara ya kwanza kwamba naondoka na wamefurahi. Awali, walikuwa wakiondoka wanatembea wameinamisha vichwa barabarani.

Mechi pekee ambayo Arsenal waliwahi kushinda dhidi ya Mourinho wakiwa na Wenger ilikuwa mwaka 2015 wakati wa mechi ya Ngao ya Jamii Mourinho alipokuwa Chelsea.

Klabu za wawili hao zilikutana mara ya kwanza Desemba 2004 – Gunners walipokuwa bado wanatumia uwanja wa Highbury – mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *