Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kiungo wake, Henrikh Mkhitaryan anahitaji muda wa kuzoea ligi ya Uingereza na mazingira yake.

Mourinho amesema anaamini kwamba Henrikh Mkhitaryan anaweza kuwa mchezaji bora wa Manchester United siku za mbele lakini anahitaji muda kuzoea mazingira ya soka la Uingereza.

Kocha huyo amemfananisha kiungo huo na mchezaji wake wa zamani katika klabu ya Chelsea kwa kusema wakati anamsajili Willian alikuwa mchezaji wa kawaida lakini baada ya kuizoea ligi ya Uingereza sasa hivi ni moto wa kuotea mbali.

Mkhitaryan mwisho kuichezea Manchester United ilikuwa mechi dhidi ya Manchester City kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza ambapo Manchester United walifungwa 2-1 katika uwanja wa Old Traford.

Kiungo huyo wa Armenia mwenye umri wa miaka 27 alisajiliwa na Manchester United kwa ada ya uamisho iliyogharimu pauni milioni 26 akitokea klabu ya Borussia Dortmund mwezi Julai mwaka huu.

Manchester United kesho inatarajiwa kucheza dhidi ya Barnley kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza katika uwanja wa Old Traford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *