Kocha wa Machester United, Jose Mourinho amesema kuwa makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward anajua wachezaji wanaotakiwa kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.

“Ed Woodward anayolisti yangu ya wachezaji ninaowataka,”alisema meneja huyo baada ya mchezo wa Europa ligi dhidi ya Ajax.

Mourinho amesema kuwa anataka kuongeza wachezaji wapya katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuweza kuwania taji la ligi kuu ya England msimu ujao.

United wamekua wakihusishwa na kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuwasajili Antoine Griezman toka Atletico Madrid ambaye tayari ameonesha nia ya kujiunga na United, Andrea Belotti wa Torino pamoja Romelu Lukaku.

Kwa upande wa safu ya ulinzi wachezaji wanaotajwa kuwa wako kwenye rada ya Mourinho ni beki wao wa zamani Michael Keane anayecheza Burnley, beki kisiki wa Benfica Victor Lindelof na Mholanzi Virgil van Dijk wa Southampton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *