Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema mshambuliaji wake Wayne Rooney atabakia kuwa mchezaji muhimu kweye kikosi hicho licha ya kumuweka benchi kwenye mechi dhidi ya Lecester City.

Kocha huyo amesema anamuamini Rooney kwa sababu ni mchezaji bora kwa United isipokuwa kwasasa kiwango chake kimeshuka lakini si sababu ya kumfanya kumumweka benchi kila mechi.

Rooney alianzia benchi kwenye mechi ya ushindi 4-1 dhidi ya Leicester City katika uwanja wa Old Trafford lakini aliingia dakika saba za mwisho za mchezo huo.

Rooney
Rooney

Bila ya Wayne Rooney Manchester United ilitumia dakika 20 kushinda kupitia kwa Chris Smalling, Juan Mata, Marcus Rashford na Paul Poga huku United ikionekana kutawala mchezo huo.

Kwa mara ya mwisho Rooney kuanza benchi kwenye mechi ya ligi nchini Uingereza ilikuwa mwaka siku ya Boxing Day.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *