Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema wapinzani wake wanaoongelea juu ya gharama ya uhamisho wa Paul Pogba kwasababu klabu zao hazina uwezo wa kununua mchezaji kwa bei hiyo.

Mourinho amesema kwamba muda mwingine kwenye mpira vitu vinatokea kama kuvunja rekodi ya usajili lakini hii peke yake inawezekana kwenye klabu kubwa kama Manchester United kwa Uingereza.

Vile vile Mourinho amesema amesikia maneno mengi kuhusu usajili huo kutoka kwa baadhi ya makocha wakikosoa lakini hakuna tatizo baada ya kukamilika kwa usajili wa Pogba.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ni miongoni mwa makocha waliokosoa gharama ya usajili huo huku kila mmoja akidai kwamba mchezaji huyo hana thamani ya bei hiyo.

Kabla ya kukamilika kwa usajili wa Pogba, Wenger amesema usajili huo ni wakipuuzi huku Jurgen Kloop akidai kwamba hawezi kutoa fedha zote kwa kununua mchezaji mmoja.

Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Manchester United hapo jana kwa uamisho uliovunja rekodi paundi milioni 89 akitokea Juventus ya Italia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *