Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazili, Neymar da Silva Santos Junior  kuhamia klabu ya Paris Saint-Germain umebadili kilakitu katika soko la wachezaji.

Mourinho anaamini kuwa United imeokoa mamilioni ya fedha baada ya kufanya usajili wake mapema kabla ya usajili wa Neymar Jr kufanyika.

PSG ilifanikiwa kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili Neymar  kwa paundi milioni 222 na kuvunja rekodi iliyowekwa na United ya paundi milioni 89.3 ya kumsajili Paul Pogba katika majira ya joto.

Kisha kufuatiwa na Barcelona kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund, Ousmane Dembele kwa ada ya paundi milioni 97.

PSG ikafanya usajili mwingine mkubwa wa kushtukiza kwa mkopo wa muda mrefu mchezaji wa Monaco, Kylian Mbappe kabla ya kuingia mkataba naye wa paundi milioni 166.

Kisha Manchester United kumsajili Romelu Lukaku kwa paundi milioni 90.

Hivyo Mourinho anaamini ameokoa kiasi kikubwa cha fedha baada ya kukamilisha usajili wake mapema mwezi Julai.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *