Kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa klabu hiyo kwa ajili ya ligi kuu nchini Uingereza iliyoanza mwezi Agosti mwaka huu.

Hapo awali kiungo huyo aliambiwa na kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho kwamba hawezi kupata nafasi tena kwenye kikosi hicho cha Mashetani wekundu wenye maskani yao Old Trafford kwa kutokana na kushuka kiwango.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aliamua kumpeleka kiungo huyo kwenye kikosi cha pili cha Mashetani hao kwa ajili ya kupandisha kiwango chake ambacho kimetetereka kwasasa.

Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kutumia timu ya taifa ya Ujerumani miaka 12 ambapo amecheza mechi 121 na kushinda magoli 24.

Schweinsteiger alisaini mkataba wa miaka mitatu mwaka jana na Manchester United chini ya kocha Louis Van Gal akitokea mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

Kwa upande wake Jose Mourinho amesema kwamba licha ya kiungo huyo kujumuishwa kikosi cha United lakini atambue kwamba Paul Pogba, Marouane Fellaini, Morgan Schneiderlin, Ander Herrera na Michael Carrick wote wapo juu yake kwenye nafasi ya kuanza.

Kikosi kamili cha Manchester United kwa ajili ya mashindano ya ligi kuu nchini Uingereza ni:

Eric Bailly, Daley Blind, Michael Carrick, Matteo Darmian, David De Gea, Memphis Depay, Sadik El-Fitouri, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Zlatan Ibrahimovic, Sam Johnstone, Phil Jones, Jesse Lingard, Juan Mata, Henrikh Mkhitaryan, Paul Pogba, Marcos Rojo, Sergio Romero, Wayne Rooney, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Chris Smalling, Antonio Valencia, Ashley Young.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *