Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kiungo wa klabu hiyo, Bastian Schweinsteiger hatoihama timu hiyo na atajumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo Europa League.

Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga goli kwenye ushindi wa United wa 4-0 Kombe la FA dhidi ya Wigan jana.

Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016 na kushinda goli.

Schweinsteiger aliachwa nje ya kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho na akalazimishwa kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 mwanzoni mwa msimu.

Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young lakini wachezaji waliobaki hawataondoka.

Schneiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye.

United watakutana na Saint-Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16 Februari, na mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *