Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa amemtaka mshambuliaji wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ili anendelee kusalia katika klabu hiyo.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Manchester United akiwa mchezaji huru kutoka Paris-St Germain kwa kipindi cha msimu mmoja huku akiwa na nafasi ya kuongeza mkataba mwingine.

Raia huyo wa Sweden amefunga magoli 26 katika mechi 38 msimu huu, ikiwemo bao mbili katika ushindi wa kombe la EFL dhidi ya Southampton.

Mourinho amesema kuwa sote tunataka asalie na tunaamini atafanya hivyo kwa msimu mwengine mmoja.

Ibrahimovic alibeba kombe hilo la 32 katika kipindi chake chote cha soka baada ya kufunga bao la dakika 87 katika uwanja wa Wembley

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *