Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa waamuzi wanaocheza mechi dhidi ya timu yake ndiyo chanzo cha kupotea mechi hizo kwenye mashindano tofauti barani Ulaya.

Jana Manchester United imepoteza mechi ya tatu mfululizo kufuatia kipigo cha 3-1 kutoka kwa Watford kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza.

Mourinho amepoteza mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza msimu huu toka Februari 2002 wakati akiwa kocha wa Porto ya Ureno.

Mourinho amesema kuwa muamuzi aliyechezesha mechi dhidi ya Watford ndiyo chanzo cha kupoteza mechi hiyo kutokana na kuacha faulo ya wazi aliyechezewa Anthony Martial na Watford kuandika golia la kwanza

Michael Oliver: Muamuzi aliyechezesha mechi ya Watford dhidi ya Manchester United.
Michael Oliver: Muamuzi aliyechezesha mechi ya Watford dhidi ya Manchester United.

Vile vile Mourinho alimshtumu muamuzi aliyechezesha mechi dhidi ya Manchester City baada ya kusema kuwa walinyimwa penati ya wazi kwenye mechi hiyo ya wapinzani wa jadi.

Baada ya kipigo cha jana kutoka kwa Watford timu hiyo ya Manchester United imeshuka mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ambapo ina alama tisa baada ya kucheza michezo mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *