Kocha mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa anataka kubakia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi kwa kuwa anapenda maisha yake na timu hiyo.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alijiunga na klabu hiyo mwezi Julai mwaka huu na sasa timu hiyo ipo katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya mechi 17.

marcus-rashford-jesse-lingard-henrik-mkhitaryan-luke-shaw-juan-mata-jose-mourinho_3750044

Mwezi Oktoba, Mourinho amesema kuwa hoteli anayoishi ni janga baada ya kikosi cha United kupata matokeo yasiyoridhisha.

Mourinho ameongezea kwa kusema kuwa hatoelekea kufunza nchini China ,ijapokuwa amekiri kwamba fedha za China zinavutia kila mtu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *