Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema mlinzi wa kati wa timu hiyo Phil Jones atakuwa fiti kuivaa Tottenham kwenye mchezo wa EPL utakaopigwa kwenye dimba la Old Traford Jumamosi hii.

Phil Jones aliumia nyama za paja kwenye mchezo wa EPL wikiendi iliyopita ambapo Manchester United ilikubali kichapo cha kwanza msimu huu kutoka kwa Huddersfield Town iliyopanda daraja msimu huu.

“Phil Jones yuko vizuri na yupo tayari kurejea uwanjani kwasababu hakuumia sana, pia mwenyewe ameniambia yupo tayari kwa mchezo ni mimi tu nikihitaji huduma yake”, amesema Mourinho.

Manchester United na Tottenham zote zina alama 20, United ikiwa katika nafasi ya pili na Tottenham nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao.

Mshindi wa mchezo huo atakuwa amemzidi mwenzake alama tatu na kuisogelea Manchester City ambayo inaongoza ligi ikiwa na alama 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *