Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Manchester City wakiwa bila mshambuliaji, Sergio Aguero.

Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amefungiwa kutocheza mechi tatu baada ya kumgonga mchezaji wa West Ham kwa kiwiko cha mkono mechi ambayo City walishinda 3-1.

Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi kuu msimu huu lakini Mourinho amesema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.

Sergio Aguero
Sergio Aguero

Mourinho amesema kwamba itakuwa vigumu zaidi kwababu Aguero akiwepo lazima utajua anacheza namba gani.

Mourinho amesema mmoja kati ya Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa kama ‘nambari tisa bandia’ kwenye debi hiyo Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *