Moto umeteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku wa kuamkia leo.

Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

Moto huo unadaiwa kuanza majira ya saa 2:00 usiku na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hizo zimefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.

Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto ingawa vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *