Moto umeteketeza godauni la kuhifadhia matairi la Kampuni ya 7 General karibu na Chuo Kikuu cha Tumaini eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na inavyoonekana moto wa matairi kuuzima siyio kazi rahisi.

Timu ya Kikosi cha Zimamoto imewahi kufika eneo la tukio ikiwa na magari takribani matano na kufanya juhudi za kuuzima moto huo lakini hawajafanikiwa.

hatari2

Mpaka sasa maji yameisha na magari mengine yamefuata maji mengine kwa ajili ya kuendelea na zoezi la uzimaji.

Picha kwa hisani ya Glabal Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *