Baadhi ya maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) yameteketea na moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha hofu kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo.

Kutokana na moto huo shughuli zote uwanjani hapo zimesitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno amesema kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za usafirishaji zimehamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *