Aliyekuwa mbunge wa Kasulu Mjini mkoani Kigoma kupitia chama cha NCCR Mageuzi, Moses Machali amehama chama chake cha ACT-Wazalendo na kuhamia chama tawala CCM.

Kupitia taarifa yake Machali amesema ameamua kuamia CCM ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na uongozi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Machali amesema kuwa mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

Pia Machali amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono.

Moses Machali aliwahi kuwa chama cha NCCR Mageuzi kabla ya kuhama na kuhamia chama cha ACT-Wazalendo na kugombea ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la Kasulu Mjini na kushindwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *