Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata anatarajia kukaa nje ya uwanja zaidi ya mwezi mmoja baada ya kupata jeraha la misuli ya paja.

Mchezaji huyo aliumia kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza katika ya Chelsea na Manchester City ambapo Chelsea walipoteza kwa kufungwa 1-0.

Morata mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Chelsea kwa £60m majira ya joto kutoka Real Madrid ada iliyovunja rekodi Chelsea.

Madaktari wa timu ya taifa ya Uhispania wanasema alipata jeraha la ngazi ya tatu kwenye misuli yake ya paka na hataweza kuwachezea mechi za kufuzu za Kombe la Dunia dhidi ya Albania na Israel wiki hii.

Majeraha kama hayo kwenye misuli mara nyingi huchukua wiki nne hadi nane kupona.Uhispania wanaongoza Kundi G wakiwa alama tatu mbele ya Italia, wakiwa wamesalia na mechi mbili.

Chelsea wamepangiwa kucheza dhidi ya Crystal Palace 14 Oktoba na baadaye dhidi ya Roma, Watford na Everton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *