Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Tiba na Mifupa (Moi), Dk Othman Kiloloma amesema kuwa kitengo hiko kipo katika mchakato wa kupunguza wafanyakazi 45 waliokutwa na vyeti feki.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofika hospitali hapo, Dk Kiloloma alisema pia taasisi hiyo ina upungufu wa fedha kutokana na Serikali kushindwa kutoa zuruku ya Sh4.8 bilioni zilikuwa zitolewe kwa mwaka wa 2016/17.

Alisema kutokana na tatizo hilo imekuwa vigumu kwao kujiendesha kwani kitengo kinatumia Sh20.6 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kununulia vifaa vya tiba pekee, wakati huo asilimia 70 ya wagonjwa wakitibiwa kwa msamaha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alisema MNH iliidhinishwa kupewa Sh4 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali lakini mpaka sasa haijapokea fedha hizo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *