Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ameisadia timu yake ya Misri kufuzu fainali za kombe la dunia baada ya kushinda kufunga goli mbili kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Congo.

Misri imefuzu kwenda fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990, mkwaju wa penati wa Salah katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza ilileta ushindi uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wa nchi nzima.

Misri imekuwa nchi ya pili kufuzu kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2018 nchini Russia baada ya Nigeria kujihakikishia nafasi siku ya Jumamosi.

Ushindi huo umepelekea maelfu ya mashabiki kujazana kwenye mitaa ya Misri wakisherekea huku wakipeperusha bendera za taifa lao.

Katikati ya jiji la Cairo helicopter ya kijeshi ilikuwa ikidondosha mamia ya bendera za nchi hiyo kwa mashabiki waliokuwa barabarani wakishangilia kwenye sehemu maarufu inayofahamika kwa jina la Tahrir square.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *