Mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu amekuwa gumzo katika mkutano mkuu wa wanachama wa Simaba uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wanachama walionekana wazi kuwa wana hamu ya kuusikia uongozi wao unasema nini kuhusiana na kuingia kwenye kampuni ambako Simba itaweza kuuza hisa.

Uamuzi huo ulisababisha wanachama kutotaka kujadili chochote zaidi ya kuona kama uongozi uko tayari kuuza hisa zake asilimia 51 kwa Sh bilioni 20 kwa Mohamed Dewji.

Wakati wa kujadili ajenda nyingine za kikao kama zile za Hesabu na Chombo cha uchaguzi hazikuwa na mvuto na wengi walitaka ajenda namba tisa ambayo ilikuwa ni Taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa uendeshaji.

Wanachama wamelalamikia uongozi ulipita huku wa Wakipiga kelele wakitaka kusikia mjadala.

Rais wa Simba Evans Avena alilazimika kurejea na kuwaeleza kwamba kama wanataka Simba kuingia kwenye mchakato wa kampuni, maoni yao yamesikilizwa na yanaanza kufanyiwa kazi.

Kauli hiyo ya Aveva ilifanya wanachama hao washangilie kwa nguvu hata yeye baada ya kuufunga mkutano huo hapo jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *