Mfanyabiashara Mohammed Dewji ametoa Tsh milioni 100 kuchangia mfuko wa usajili wa klabu ya Simba ambaye ana dhamira ya kununua asilimia 51 ya hisa kwenye timu hiyo.

 Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Mohammed Dewji alitangaza mpango wake wa kununua hisa Simba, huku akisema kama mkutano mkuu wa Simba uliofanyika Julya 31 mwaka huu wakikubali mfumo wa mabadiliko ya utawala na klabu ikaendeshwa kwa mfumo wa hisa, atasaidia mfuko wa usajili wa Simba.

Mohamed Dewji amekabidhi kiasi hicho cha fedha kwa katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele na Rais wa Simba Evans Aveva mbele ya waandishi wa habari.

Dewji amekabidhi hundi ya Tsh Milioni 100 kama sehemu ya kutimiza ahadi yake, kati ya zaidi Tsh Milioni 400 ambazo ni bajeti ya usajili yaSimba msimu huu, akiuziwa asilimia 51 ya hisa Simba.

Vile vile Dewji ameahidi bajeti ya usajili ya klabu ya Simba itakuwa zaidi ya Tsh Bilioni 1 kwa mwaka.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *