Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobetto amepata dili nono la ubalozi wa vipodozi vya Whitenicious kwa upande wa Bara la Afrika akimsaidia mwanadada Blac Chyna ambaye ni Balozi wa bidhaa hizo.

Akiweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa Mobetto ameandika kuwa “Hatimaye siri ya urembo wangu ni hii. Ningependa kutangaza rasmi kwamba nimekuwa balozi wa Whitenicious Afrika.

Kwa kushirikiana na Whitenicious nitatangaza urembo kwa kutumia bidhaa za asili kwaajili ya wanaume na wanawake.

Kwa miaka mingi Afrika imekuwa ikipokea bidhaa za urembo zenye kemikali. Bidhaa hii inamiaka 30 sokoni ikihakikisha ngozi za wanawake na wanaume zikiwa salama”.

Milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa mwanamitindo huyo kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa hizi za urembo za kimataifa pia ni balozi wa kinywaji cha kishua cha Belaire.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *