Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika comment ilionekana kumlenga Linah ambapo pia Lina alijibu comment hiyo.

Moja ya picha Linah alizopost hivi karibuni akiwa na baba wa mtoto wake,katika posti hiyo ambayo inaonekana kama kama kuna siri chini ya kapeti kuhusu uwepo wa mwanamke mwingine mjamzito mwenye mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie na Linah.

Katika post hiyo Hamisa aliandika”lv unajua kuwa kuna mwenzio ana mimba$$$ mdomo koma lakini” maneno haya yanayoonyesha kama kuna kitu Hamisa anajua kuhusu mwanamke huyo mwingine mwenye mimba hivyo inakuwa kama anatoa tarifa kwa Linah.

Lakini kitu cha kushangaza ni jinsi Linah alivyamua kumjibu Hamisa kuhusu taarifa hizo ambapo anaonyesha kujua kwa taarifa hizo na anaonekana kutokujali kuhusu maneno hayo” @ hamisamobetto, Najua, tulishayaongea kuna lingine” alijibu linah

Linah Sanga ambae miezi michache iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kike mwenye jina TracyParis aliezaa na mpenzi wake  , alisikika hivi karibuni akisema kuwa yeye na mzazi mwenzie huyo wanategemea kufunga ndoa ukiachalia mbali tofauti zao za kidini .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *