Staa wa wa Bongo Fleva, MO Music amefunguka kwa kusema kuwa sababu ya kundi la Wazawa kuvunjika ni ugomvi binafsi wa T Nocks na Baraka The Price ndiyo uliopelekea kundi hilo kuvunjika.

Mo Music alikuwa ni memba wa kundi hilo lililokuwa likiundwa na wasanii kutoka Mkoa wa Mwanza lililojulikana kwa jina la WAZAWA, lililokuwa likiundwa na yeye (MO Music), Baraka The Prince pamoja na T Nocks.

Mo aliongeza kwa kusema kuwa “Kila mtu ana akili zake tofauti na utofauti huo ndiyo uliopelekea Wazawa kushindwa kudumu, mara nyingine miongoni mwetu wengine walikuwa wanajiona bora zaidi ya wengine”.

Pia Mo Music aligusia kwa kusema sababu ya ugomvi wa Baraka na T Nocks kuwa ni wimbo wa So Fly, wimbo ambao ulimtambulisha Baraka vizuri hasa kwa mkoa wa Mwanza.

Baraka The Prince
Baraka The Prince

Mwanamuziki huyo kwasasa anafanya muziki kama solo artist ambapo ametoa nyimbo ambazo zilifanya vizuri katika anga za muziki wa Bongo fleva kama vile ‘Nitazoea, ‘Skendo’ na ‘Ado Ado’.

Kwa upande wa aliyekuwa memba mwenzie wa kundi hilo Baraka The Prince anafanya vizuri kuliko Mo Music kutokana na nyimbo zake kuonekana kufanya vizuri kwenye media mbali mbali hapa nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *