Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kufanya Mkutano wa Mabadiliko ya katiba utakaofanyika siku ya Jumapili ya Mei 20, 2018.

Kwa mujibu wa afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram ameandika kuwa wanakwenda kukamilisha mchakato rasmi tarehe 20 mwezi huu.

Mkutano huo unaashiria kukamilika kwa mabadiliko hayo ya katiba kutampa wepesi mshindi wa dhabuni ya timu hiyo, Mohammed Dewji kukabidhiwa majukumu rasmi.

Ameandika Tunakwenda kukamilisha mchakato rasmi tarehe 20 mwezi huu..Mpira ni pesa sio porojo za kutegemea kuuza majarida..na uzuri wake MO anakuja kuwekeza pesa..ni pesa tu…..tunahesabu siku tubadilishwe hadhi.

Uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa kuwa unatarajia kufanya mkutano wake wa dharura Mei 20 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *