Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ameshinda tuzo ya mtu aliyefanya vizuri katika Uongozi kwa Mwaka 2016 inayotolewa na Jarida la African Leadership.

Dewji  ameibuka na ushindi huo kwa kupata kura asilimia 60.8 dhidi ya John Mahama,Rais mstaafu wa Ghana aliyepata kura 30.2 na kuwa mshindi wa pili.

Watu zaidi ya 89,055 na kutazamwa na watu zaidi ya milioni 2.1 kwenye mtandao na nje ya mitandao kwenye Jukwaa la Jarida la African Magazine.

Kiongozi huyo wa Makampuni ya MeTL Group ameibuka mshindi katika mchuano mkali uliohusisha watu maarufa barani Afrika ikiwa ni pamoja na mwanzilishi wa kampuni ya ECONET Wireless,Mkenya,Chris Karubi,Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika,Akinwumi Adwesina,Naibu Rais, Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na Waziri wa Mazingira wa Nigeria na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Aisha Mohammed.

Dewji atatunukiwa rasmi tuzo hiyo katika sherehe itakayofanyika Februari 24, mwaka huu katika Hoteli ya Southern Sun mjini Pretoria nchini Afrika Kusini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *