Mohammed Dewji maarufu kwa jina la ‘MO’ amefanikiwa kushinda tuzo kutoka Taasisi ya Choiseul ya nchini Ufaransa kama mfanya biashara kijana ambaye anasaidia kukuza uchumi wa bara la Afrika.

Dewji  ameshinda tuzo hiyo ambayo aliwashinda wafanyabiashara wengine vijana 100 wenye asili ya Afrika ikiwa ni mara ya tatu kushinda tuzo hiyo tangu taasisi hiyo ianze kutoa tuzo hiyo.

Choiseul imesema kuwa Mohammdei Dewji amekuwa akijihusisha kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko na kutoa nafasi kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi jambo ambalo limeleta matumaini mapya kwa Tanzania na Afrika kuweza kufika pale wanatamani wafike.

Kwa upande wake Dewji amesema kuwa ataendelea na dhamira yake ya kuisaidia Afrika kupitia biashara anazozifana.

Mohemed Dewji ni mfanyabishara maarufu hapa nchini amejizoela sifa maeneo mbali mbali ya bara la Afrika kutokana na uzalishaji wake katika sekta ya kilimo pamoja na usambazaji wa bidhaa katika Bara la Afrika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *