Mmiliki wa shule ya Lucky Vincent ambaye anatambulika kwa majina ya Innocent Mushi leo amefikishwa mahakamani  jijini Arusha.

Mmiliki wa Shule huyo amesomewa mashtaka manne na kuachiwa kwa dhamana kutokana na kosa lake.

Baada ya kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka hayo, mahakama hiyo imewaachia huru mmiliki wa shule Innocent Mushi na Makamu Mkuu wa shule hiyo Logino Vicenti kwa dhamana ya Sh15m kila mmoja.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani leo, baada ya gari yao aina ya ‘coaster’ kusababisha vifo vya watu 35.

Basi hilo liliua idadi kubwa ya watu hao baada ya kutumbukia katika korongo na kukatisha uhai wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent Nursery & Primary School 32, walimu wawili wa shule hiyo pamoja na dereva ambaye alikuwa akiendesha gari hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *