Maafisa usalama wa kinyuklia nchini Ufaransa wamethibitisha kutokuwepo kwa tishio lolote la nyuklia kufuatia mlipuko na moto kutokea kwenye kinu cah nyuklia cha Flamanville, nchini humo.

‘Ni tukio muhimu la kiufundi lililojitokeza lakini sio ajali ya nyuklia’. Amesema afisa kiongozi wa kinu hicho Olivier Marmion.

Kufuatia tukio hilo, shirika la habari la AFP limeripoti kuwepo kwa watu watano ambao hawajisikii vizuri ingawa hakuna aliyejeruhiwa sana.

Kinu cha Flamanville kina sehemu mbili za kutengenezea nyuklia wakati huo huo sehemu moja zaidi ikiwa kwenye matengenezo.

Hata hivyo chanzo cha mlipuko huo bado hakijatajwa kwa haraka.

Mwaka 2015, udhaifu unaoaminika kuwa ni kosa lililotokea wakati wa ujenzi liligundulika na kushughulikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *