Muigizaji wa maigizo ya vichekesho, Hemed Maliaga maarifu kwa jina la ‘Mkwere’ amempa ushuri wa kuishi na mke vizuri rafiki yake Crispine Lyogello maarufu kama ‘Masele Chapombe’ baada ya kufunga ndoa wiki iliyopita.

Mkwere aliyasema hayo alipoombwa kutoa ujumbe wowote siku ya harusi hiyo, jambo lililomfanya atokwe machozi katika kusimulia njia waliyopitia.

Mkwere alisema yeye na Masele wamekuwa wakishirikiana tokea wakiwa wanatafuta maisha ambapo walisota na kukaza mikanda hadi kuyafikia mafaniko ya kujulikana katika tasnia ya komedia nchini

Mkwere alitokwa na machozi pale alipopewa nafasi ya kusema chochote kuhusu rafiki yake huyo ambapo alisema alikumbuka mamabo mengi tangu walipoanza kutafuta maisha kupitia sanaa.

Ndoa hiyo imefufungwa mwezi huu kanisani  Mbezi-Kimara jijini Dar es Salaam ambayo ilifuatiwa na tafrija ya nguvu katika ukumbi wa Mbezi Luxury.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *