Mkwasa: Sijapokea barua ya kujiuzulu kwa Manji

0
351

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa bado hajapokea taarifa za kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Mkwasa amesema kuwa hajapata taarifa rasmi juu ya ukweli wa suala hilo kwasabu bado hajawasiliana na Manji kama kweli amechukua uamuzi huo.

Katibu mkuu huyo amesema hayo baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Manji ameandika barua ya kujiuzuru cheo hicho ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema kuwa yeye kama mtendaji mkuu wa klabu hiyo bado hajakabidhiwa barua ya kujiuzuru kwa Manji kutokana na hafanyi kazi katika mitandao kwa hiyo mpaka akipata ufafanuzi kuhusu suala hilo ndiyo ataliongelea.

Mkwasa amesema “Tunajua kuwa mitandaoni kuna taarifa nyingi ambazo siyo za kweli na zipo nyingine ambazo zimesababisha baadhi ya wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hivyo nasubiri kuona kama ni kweli, basi nitapatiwa barua rasmi na nitatoa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo.”

Alipoulizwa kama amewasiliana na Manji hivi karibuni, alisema: “Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa njia ya barua pepe kwa masuala ya kiofisi lakini sijakutana naye siku mbili hizi.”

Leo kumekuwa kukisambaa barua ambayo inaonekana imesainiwa na mwekiti huyo akielezea uamuzi wake wa kutangaza kujiuzulu ndani ya klabu ya Yangu.

LEAVE A REPLY