Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Nigeria katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kocha huyo amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti.

Mechi hiyo ya Taifa stars na Nigeria “Super Eagles”  inatarajiwa kuchezwa jijini Lagos nchini Nigeria Septemba 2, mwaka huu.

Taifa Stars imepangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika nchini Gabon, mwaka 2017.

 Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kuongoza kundi hilo na kukusanya alama 10, Nigeria ina alama mbili, Taifa Stars alama moja wakati Chad imejitoa katikati ya mashindano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *