Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amesema kuwa Rais Yahya Jammeh atakubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika jana.

Amesema kuwa si jambo la kawaida kwa rais wa Gambia kukubali kushindwa kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.

Hata hivyo hakuna taarifa yoyote kutoka kwa bwana Jammeh ambaye amekuwa nyuma ya kiongozi wa upinzani Adama Barrow kwenye matokeo ya kwanza

Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994 kufuatia mapinduzi ya kijeshi na sasa anawania muhula wa tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *