Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM kwenye mahafali ya kidato cha nne.

Mkuu huyo wa shule pia alipinga kitendo cha baadhi ya walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta michango yote mashuleni.

Mkuu huyo nadaiwa kushushwa cheo kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, ambaye amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.

Taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *