Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Waliosimamishwa kazi ni Mweka Hazina Evance Mwalukasa, Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Sembele Siloma na Ofisa Uchaguzi wa jimbo hilo, Khadija Mkumbwa.

Wanaotakiwa kurudi Arusha na kujibu tuhuma zinazowakabili ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ngorongoro, Mgalula, Ofisa Mipango Aloyce Chambi, Ofisa Elimu Shule za Msingi, Natangiapo Mollel na Mhandisi Benjamini Maziku.

Mkuu wa mkoa huyo amechukua uamuzi huo baada ya kukamilika kwa taarifa ya kamati yake, aliyounda yenye wajumbe watano iliyochukua wiki mbili na aliisoma taarifa hiyo mara baada ya kuzungumza na watumishi wa halmashauri na watendaji wa kata kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Amesema Mweka Hazina na Mwanasheria, walishindwa kumshauri vizuri mkurugenzi kuwa malipo ya Sh milioni 135 zilizokuwa zikilipwa nje ya mwongozo na Sh milioni 20 zilizotumika katika manunuzi kinyume cha utaratibu.

Pia aliongeza kusema mwanasheria huyo kwa mara nyingine, aliruhusu kiholela bila ya kufuata Sheria ya Manunuzi na Ugavi kulipa zaidi ya Sh milioni 180 kwa malipo ya magari 18 katika kipindi cha uchaguzi. Mbali ya hilo, kamati hiyo ya uchunguzi ilibaini kuwa watumishi wa halmashauri hiyo, walijilipa posho zaidi ya Sh milioni 20 kinyume cha utaratibu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *