Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo ameahirisha kufanya mazungumzo na wazee wa Kibiti.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amesema ni kutokana na mkuu huyo kupangiwa majukumu mengine ya kikazi.

Awali, Mabeyo alitarajiwa kufika Kibiti kufanya mazungumzo na wazee kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama mkoani humo ambamo kumekuwa na mfululizo wa mauaji hasa ya viongozi wa vijiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *