Waandishi wa habari wamepigwa na butwaabbaada ya mkutano aliotakiwa kuufanya Roma Mkatoliki na waandishi wa habari kushindwa kufanyika kwa wakati.

Mapema leo kaka yake Roma, Omary Musa amesema mkutano huo ungefanyika saa tano kamili asubuhi ya leo.

Hata hivyo Musa hakuweka wazi eneo la kufanyia mkutano huo kwa kile alichodai bado hawajapata eneo.

Ilipofika saa tano mwandishi alimtafuta kujua eneo Musa akajibu bado hawajapata na huenda mkutano huo ungesogezwa hadi saa nane.

“Bado tunatafuta kuna watu wamepewa jukumu hilo, hatuwezi kufanyia popote lazima liwe eneo salama, hatujui waliomteka walikuwa na nia gani”

“Nipigie baada ya dakika 45 nitakuwa nimeshajua, muhimu kuweni na subira tutawataarifu,” amesema

Jumamosi iliyopita baada ya kupatikana akiwa kituo cha polisi Osterbay Roma aliahidi kuzungumza na waandishi leo kuelezea kilichotokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *