Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, amewatangazia wanachama na wapenzi wa klabu hiyo  kwamba kutakuwa na mkutano mkuu wa timu utakaofanyika Jumamosi Agosti 6.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema mkutano huo umepangwa kufanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo amesema wanachama wote hai waliolipia kadi zao za uanachama, wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha mkutano huo.

Mkutano huo unakuja baada ya siku chache tangu klabu ya Simba ifanye mkutano wake mkuu pamoja na wanachama wake na kufikia baadhi ya makubaliano ikiwemo kuboresha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Vile vile Yanga inatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku hiyo hiyo ya jumamosi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *