Rais John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felschemi Mramba kuanzia leo, Januari 1, 2017.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Dkt. Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo. Kabla ya uteuzi huo,  Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Hatua hiyo inafuata baada ya siku moja waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo kusitisha bei mpya ya umeme ilitangazwa na EWURA ambao walipata ombi kutoka TANESCO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *