Mkurugenzi mtendaji na mmiliki wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo ameachiwa huru kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Melo anakamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam tangu Jumanne iliyopita kwa madai ya kugomea agizo la muda mrefu la jeshi hilo.

Mkurugenzi huyo wa Jamii Forum alisomewa makosa 3 likiwemo la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa ambapo ni kinyume na sheria.

Shitaka lingine ni kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao pamoja na kusajili tovuti ya Jamii Forums kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo serikali inadai ni kinyume cha sheria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *