Partners: Babu Tale Said Fella a.k.a Mkubwa Fella
Washkaji: Babu Tale Said Fella a.k.a Mkubwa Fella

Meneja wa familia ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella amekubaliana na kauli iliyotolewa na rapa mtata, Roma Mkatoliki kwenye ngoma yake mpya ‘KAA TAYARI’ ambapo anadaiwa kum-dis meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale kwenye mstari anaosema ‘Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top’.

Babu Tale ni meneja wa kundi la Tip Top Connection na pia ni meneja wa Diamond Platnumz ambaye moja ya a.k.a zake ni ‘Dangote’.

Mkubwa Fella amedai kuwa aliwahi kumtahadharisha Babu Tale juu ya jukumu lake kwa Tip Top Connection ambayo kwa sasa imepotea kwenye ramani ya Bongo Fleva huku wasanii wake Madee na Dogo Janja pekee wakiwa wanasikika.

Meneja hewa?: Babu Tale (K) akiwa na Diamond Platnumz a.k.a Dangote
Meneja hewa?: Babu Tale (K) akiwa na Diamond Platnumz a.k.a Dangote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *