Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Livepool, John Barnes amewasili nchini Tanzania kwa ziara maalumu.

Alipokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said ,Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 100 ya benki ya Standard Chartered ambayo ni wadhamini wakuu wa klabu ya Liverpool. .

Kwenye kusheherekea maadhimisho hayo kutakuwa na mashindano ya mpira ambapo bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda Uingereza katika jiji la Liverpool.

Timu zilizoingia fainali za mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.

Barnes ambaye hii ni zaidi ya mara ya tatu anakuja Tanzania kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *