Muimbaji Sarah Ikumu wa Uingereza mwenye asili ya Kenya amevutia watu kwenye mitandaoni ya kijamii baada ya kuimba wimbo kwenye shindano la vipaji la Uingereza la Britain’s Got Talent.

Sarah Ikumu, 16, aliyezaliwa Uingereza, aliwashangaza wengi katika kipindi cha vipaji cha Britain’s Got Talent, alipoimba wimbo wa And I’m Telling You ambao unadaiwa kuwa mgumu sana kuuimbwa ipasavyo.

Wimbo huo wake Jennifer Holliday ulitumiwa kwenye filamu ya Dreamgirls iliyotolewa mwaka 2006.

Uimbaji wa Sarah uliwaacha waliohudhuria mashindano hayo wakiwa wameduwaa huku wote wakisimama na kumshangilia.

Kilele cha uimbaji wake kikifika pale mmoja wa majaji ambaye anajulikana kuwa mgumu kufurahisha, Simon Cowell, alipobonyeza kengele ya dhahabu ambayo humpeleka mshiriki moja kwa moja hadi nusu fainali ya mashindano hayo.

Sarah ambaye anasomea Milton Keynes alianza kuimba akiwa na miaka mitano huku akishiriki kwa mashindano kadha ya nyimbo.

Lakini hili ndilo shindano la kwanza ambalo anasema kuwa ni ndoto ambayo imetimia, mwanzo pale Jaji Simon alipompongeza kwa talanta yake akimuambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *