Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa idadi ya watu wanaotumia dawa za kulevya imeongezeka kwa kipindi cha miezi miwili hadi kufikia 1,000 kutoka 644.

Profesa Manyele amesema pia wanatarajia kupokea kesi za aina hiyo 3,600 hadi kufikia Desemba mwaka huu.

Kesi hizo hivi sasa inawalazimu kwenda Kwa Mpiga Chapa wa Serikali kuchukua karatasi za siri ili kuepuka kuvuja kwa majibu hayo na wafanyakazi kulipwa malipo ya ziada kutokana na kufanya kazi kwa saa 18.

Takwimu hizo za Mkemia Mkuu zimekuja muda mfupi baada ya hivi karibuni Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya  ambapo katika orodha hiyo aliwataja baadhi ya wasanii, wanasiasa, viongozi wa dini na wafanyabiashara.

Profesa Manyele amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya serikali kuhusu ununuzi wa  mtambo wa kisasa wa kupima sampuli tofauti unaoitwa ‘energy Dispersive X-Ray Flourescence SPectrometer’ (EDXRF) ambao umegharimu Sh milioni 101.7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *