Mke wa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, Melania, na mwanae Barron hawatahamia ikulu ya White House mjini Washington DC Januari mpaka atakapomaliza shule jijini New York.

Bw Trump amesema wawili hao hawataweza kuhama katikati ya mwaka wa shule.

Alikuwa akiongea na wanahabari waliokusanyika katika kilabu chake cha gofu cha Bedminster, New Jersey Jumapili ambapo alikuwa anakutana na maafisa wanaotarajiwa kujiunga na utawala wake.

Amesema yeye ataishi White House lakini mkewe Melania Trump na Barron mwenye umri wa miaka 10 atahama “punde atakapomaliza masomo.”

Trump kwa sasa huishi na mkewe na mwanawe huyo wa kiumbe katika chumba kilicho juu kwenye jumba la ghorofa la Trump Tower jijini New York.

Barron husomea shule ya kibinafsi iliyopo jiji la New York.

Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.

Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7.

Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *