Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump na mtoto wake wamehamia Ikulu ya Marekani ya White House miezi matano tangu Donald Trump kuingia ofisini.

Melania Trump na mtoto wake wa kiume wa umri wa miaka 11 Baron walikuwa wamebaki mjini New York ili kumuwezesha kumaliza masomo ya mwaka katika jiji hilo.

Hatua hiyo imekuwa ya kushangaza kwa wengi kwa kuwa ndiyo familia ya kwanza miaka ya hivi karibuni kukosa kuhamia Ikulu ya White House mara moja.

Mtangulizi wake Michelle Obama hata alhamia White House, mapema kuwezesha watoto wake kujunga na shule mapema.

Hata hivyo inaonekana kuwa Melania amefurahishwa na hatua yake kuhamia White House baada ya kuandika kwenye Twitter alipowasili.

Trump si rais wa kwanza wa Marekani hivi karibuni kuhamia White House akiwa na watoto wa umri wa kwenda shule.

Rais Barack Obama alipoingia madarakani, mabinti wake Malia na Sasha walikuwa na umri wa miaka 10 na 7.

Rais Bill Clinton alipohamia ikulu Washington, Chelsea Clinton alikuwa na miaka 12 wakati anakuwa rais wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *