Stara Sudi ambaye ni mke wa Said Mrisho aliyetobolewa macho na Scorpion leo ametoa ushahidi mbele ya mahakama ya wilaya ya Ilala kwenye kesi ya unyang’anyi inayomkabili Scorpion.

Mke huyo wa Said Mrisho pamoja na shemeji yake Yahaya Kisukali wametoa ushahidi mahakamani kufuatia kesi hiyo inayoendelea mahakamani hapo.

Mtuhumiwa Salum Njwete ‘Scorpion’ alifikishwa mahakama hapo mida ya saa mbili asubuhi na Scorpion kufikishwa mahabusu ya mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri kesi yake kutajwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilzwa saa tatu na nusu mbele ya hakimu Flora Haule ambapo Wakili Mwandamizi wa Serikali aliielezea mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya mashahidi wawili wa upande wa serikali.

Baada ya kuweka wazi hayo kwa kuwa shahidi wa kwanza alikuwa ni majeruhi mwenyewe ambaye alishatoa ushahidi wake kesi iliposikilizwa mara ya mwisho hivyo leo ilikuwa ni siku ya shahidi wa pili, Stara Sudi na ambaye ni mke wa   majeruhi na shahidi wa tatu Yahaya Kisukari ambaye ni mdogo wa majeruhi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 11 mwakani itakapotajwa tena ambapo mashahidi wengine wa upande wa serikali watatoa ushahidi wao.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *