Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amesema kuwa serikali itashirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wazee na watu wenye ulemavu wanapata huduma za kijamii haraka iwezekanavyo.

Mama Magufuli amesema hayo mara baada ya kutembelea Kituo cha kulelea wazee cha Funga Funga kilichopo Morogoro mjini, na kutoa msaada wa chakula ukiwemo unga kilo 1300, mchele kilo 1300, maharage kilo 570, mafuta ya alizeti lita 260, sukari kilo 260 pamoja na boksi moja la mafuta kwa wazee wenye ualbino.

Aidha amewaomba watumishi wa kituo hicho kukitumia vizuri chakula hicho, kutokana na viongozi wengine ambao ni watumishi wa vituo kama hicho, kutokuwa waadilifu, kutokana na kuuza chakula cha msaada unaotolewa kwa ajili ya kuwasaidia wazee wenye uhitaji.

Hata hivyo amewashukuru wadau mbambali ambao wamejitolea, kuwachangia wazee hao, huku akiziomba taasisi za serikali, mashirika ya watu binafsi, na watu wote wenye mapenzi mema kujitahidi kuwasaidia wazee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *