Baada ya kutuhumiwa kumpiga na kumjeruhi msichana wa miaka 20 nchini Afrika Kusini, mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe hajulikani halipo hadi sasa.

Kufuatia tukio la kutoweka kwake maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wametoa tahadhari dhidi ya bi Grace Mugabe katika mipaka ya taifa hilo.

Ametuhumiwa kwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .

Polisi wanatariaji kwamba Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 52 alipaswa kujisilimisha mbele yao siku ya Jumanne lakini akakataa kufanya hivyo.

Bi Grace mugabe kwa sasa hajulikani yu wapi lakini inaaminikwamba bado yupo Afrika Kusini.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amewasili nchini Afrika Kusini kwa kikao cha viongozi wa mataifa ya Afrika Kusini SADC unaotarajiwa kuanza siku ya Ijumaa.

Polisi wa Afrika Kusini tayari wameweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *